Categories
Michezo

Wageni NAPSA Stars watua huku wenyeji Gor wakiwa mgomo

Kikosi cha wachezaji na maafisa wa klabu ya mamlaka ya uzeeni nchini Zambia NAPSA Stars kiliwasili jijini Nairobi Jumatano jioni tayari kwa mkumbo wa kwanza wa mechi ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe  la shirikisho la soka barani Afrika dhidi ya mabingwa wa Kenya Gor Mahia mchuano utakaopigwa Jumapili hii katika uwanja wa Nyayo.

Kikosi cha NAPSA kilichowasili kinawajumuisha wachezaji wawili wa humu nchini Shaban Odhonji zamani akiwa na Mathare United na Difenda wa zamani wa Gor Mahia David Owino lakini Mkenya mwingine Andrew Tololwa hakusafiri na timu himu hiyo.

Wakati uo huo wenyeji Gor Mahia walikuwa kwenye mgomo baradi na kudinda kuhudhuria mazoezi katika uwanja wa Camp Toyoyo wakiteta kuhusu kutolipwa malimbikizi ya mshara wa miezi miwili.

Wachezaji wa Kogalo wamekuwa wakigoma kabla ya kila mechi ya kimataifa kuanzia mwaka jana .

Kikosi cha NAPSA kilichowasili kinawajumuisha:-

Makipa

Philip Banda, Rabson Muchelenganga and Shabaan Odhonji

Mabeki

David Owino, Luka Banda, Luka Nguni, Aaron Kabwe, Lawrence Chungu, Bornwell Selengo, Amos Simwanza

Viungo

Jacob Ngulube, Daniel Adoko, Simon Nkhata, Dickson Chapa, Danny Silavwe, Enock Sabumukama, Austin Banda, Aaron Banda

Washambulizi

Chanda Mushili,  Laudit Mavugo, Jimmy Mukeya,  Doisy Soko, Tapson Kaseba

NAPSA watakuwa wakifanya mazoezi Alhamisi na Ijumaa katika uwanja wa Kasarani kabla ya kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza katika uwanja wa taifa wa Nyayo siku ya Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *