Wafuasi wa chama cha upinzani EFF nchini Afrika Kusini waandamana

 

Wafuasi wa chama kikubwa cha upinzani nchini Afrika Kusini EFF walifanya maandamano na kulazimisha wenye maduka ya dawa vipodozi kwa jina “clicks” kufunga maduka yao.

Lililowakera wafuasi hao wa EFF ni tangazo la kibiashara ambalo linaonekana kulinganisha nywele ya mtu mweusi na ile ya mtu mweupe. Kwenye tangazo hilo nywele ya mtu mweusi inaonyeshwa kuwa mbaya imeparara ilhali ya mtu mweupe ni ya kupendeza na imenyooka.

Kiongozi wa chama cha EFF Julius Malema anasema tangazo hilo ni la kubagua mtu mweusi kwa kumuonyesha kuwa chini kuliko mtu mweupe.

Wenye maduka hayo ya dawa na vipodozi wametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya chama cha EFF na Malema aliwarai wafuasi wa chama hicho wajiandae kufunga maduka ya clicks katika sehemu tofauti za nchi hiyo.

Jambo hilo lilizungumziwa sana kwenye mtandao wa twitter nchini Afrika Kusini ambapo watu walihimizana kususia maduka ya clicks. Kapuni ya clicks ililazimika kuomba msamaha kwenye twitter.

“Tumefanya makosa na tunaomba msamaha. Tunaelewa tuna jukumu la kuhakikisha wote wana nafasi sawa nchini Afrika kusini,kuanzia kwa yaliyo kwenye tovuti yetu. Tunajua tunafaa kujitahidi zaidi na tunajitolea kuhakikisha matoleo yetu yanaonyesha hili. “

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *