Wafanyibiashara wa shanga Kajiado wakumbatia mtandao kuuza bidhaa zao

Baadhi ya kina-mama kutoka jamii ya  Waasai ambao hujihusisha na utengenezaji bidhaa za shanga pamoja na uchuuzi katika kaunti ya Kajiado, wameanza kutumia teknolojia ili kuwawezesha kuuza bidhaa zao badala ya kuendeleza uchuuzi kwenye miji.

Kina-mama hao ambao wamekuwa wakiwauzia watalii bidhaa hizo katika mji wa mpakani wa Namanga, sasa wanatumia teknolojia kuendeleza biashara baada ya kusitishwa kwa shughuli za usafiri kufuatia janga la  COVID-19.

Mary Kilitu amesema matumizi ya simu ya rununu katika kuuza bidhaa zao na kuweza kupata pesa kwa njia ya simu imewawezesha kuendeleza biashara hiyo.

Wafanyibiashara, Sarah Kiria na Tipet Thomas wametoa wito wa kupewa mikopo kuwawezesha kupanua biashara zao.

Wamesema kuzuka kwa ugonjwa wa Covid-19 umesebabisha wao kukosa mapato.

Hata hivyo changamoto kuu kwa kina mama hao ni ukosefu wa elimu lakini wamekuwa wakijizatiti kwa kuhudhuria elimu ya watu wazima ili kujiimarisha.

Wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kajiado kuwapa mafunzo jinsi ya kutumia rununu za kisasa na pia kuwapa mikopo ili wanunue vifaa vingine vya kiteknolojia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *