Categories
Habari

Wafanyibiashara Ngara wakadiria hasara baada ya vibanda vyao kubomolewa

Takriban wafanyabiashara 500 kando kando ya barabara ya Desai katika eneo la Ngara jijini Nairobi,wanakadiria hasara, baada ya vibanda vyao kubomolewa Alhamisi asubuhi.

Wafanyabiashara hao,ambao wamekuwa wakiendesha biashara yao katika ardhi hyo ya shirika reli nchini kwa miaka kadhaa,wamesema hawakupewa muda wa kutosha kuhama.

Mmoja wa wafanyabiashara hao kwa jina Tom Otieno, amesema amekuwa akifanya biashara katika sehemu hiyo kwa miaka 18 iliyopita, na kwamba amekuwa  akilipa kodi kwa shirika la reli nchini.

Kulikuwa na aina tofauti ya biashara katika sehemu hiyo. Wafanyabiashara hao wanasema wamepoteza mali ya thamani ya mamillioni ya pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *