Wafanyibiashara ndogo ndogo watakiwa kulenga soko la Afrika Mashariki

Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa hapa nchini (KEBS) limetoa wito kwa wafanyabiashara ndogo ndogo kujipatia alama ya ubora wa bidhaa zao.

Shirika hilo limesema hatua hiyo itawasaidia wafanyabiashara hao kuuza bidhaa zao katika jumuia ya Afrika Mashariki, chini ya mkataba wa soko la pamoja.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bernard Njiraini, shirika hilo lina mpango wa pamoja wa kutambua alama za ubora wa bidhaa, chini ya mkataba wa soko la pamoja la jumuia ya Afrika Mashariki, kwa lengo la kupanua soko hilo.

Amesema hatua hiyo itasaidia wafanyabiashara ndogo ndogo nchini Kenya, kuuza bidhaa zao katika mataifa wanachama wa jumuia ya Afrika mashariki, na pia kusaidia shirika la KEBS kuchunguza bidhaa zinazoagizwa kutoka mataifa mengine.

Vile vile Kulingana na Njiraini, hatua hiyo itasaidia kudhibiti hali ya kumiminika kwa bidhaa za ubora wa kiwango cha chini hapa nchini.

Njraini alikuwa akiongea katika shule za upili za Mururia, na Ndarugu, ambako shirika la KEBS lilitoa barakoa , sabuni , mafuta ya kupikia na matangi, miongoni mwa bidhaa nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *