Wachezaji wa Gor Mahia wagoma

Wachezaji wa Gor mahia wangali wamesusia mazoezi wakitaka walipwe mshahara wao wa miezi mitatu huku wakitishia kutocheza mchuano wa marudio raundi ya kwanza kuwania ligi ya mabingwa Januari 5 dhidi ya mabingwa wa Algeria CR Belouizdad.

Yamkini wachezaji hao ambao pia walitaka kususia  mkumbo wa kwanza wa mechi hiyo mjini Algiers  hawajaripoti mazoezini tangu warejee nchini mapema wiki hii kutoka Algeria walikopoteza mabao 6-0  .

Gor watahitaji ushindi wa mabao  7-0 dhidi ya   Belouizdad   katika mechi ya wiki ijayo ili kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia.

Usimamizi wa Gor Mahia unakabiliwa na kibarua kigumu cha kufanya ili kuhakikisha mgomo wa wachezaji unamalizika ili kutoathiri matokeo yao katika hata mechi za ligi kuu zijazo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *