Categories
Habari

Wabunge na maseneta kurekebisha sheria ya ugavi wa mapato juma lijalo

Wabunge na maseneta wanatarajiwa kufanyia marekebisho sheria kuhusu ugavi wa mapato juma lijalo ili kuziwezesha kaunti kupata asilimia 50 ya mapato iliyotengewa serikali za kaunti.

Mabunge hayo mawili yanatarajiwa kutafuta suluhu ya muda ili kuwezesha kaunti kuendelea na shughuli zao huku mjadala ukiendelea wa kutafuta mfumo ufaao wa ugavi wa mapato.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei amesema kwamba, ikiwa mswada huo utashindwa basi bunge hilo halitakuwa na budi ila kupiga kura ya kupinga ama kuidhinisha mfumo mpya uliopendekezwa na kamati ya bajeti wa ugavi mapato.

Haya yanawadia wakati magavana wakitishia kufadhili bungeni hoja ya kuvunjwa kwa bunge la seneti mbali na kusitisha shughuli za serikali za kaunti.

Aidha spika wa bunge la taifa Justin Muturi ametoa wito kwa kiongozi wa walio wengi na mwenzake wa walio wachache kushauriana na maseneta wenzao kuhusiana na sheria kuhusu mswada wa usimamizi wa fedha za umma wa mwaka wa 2019 na kutathmini uwezekano wa kufanyiwa marekebisho ikiwa kuidhinishwa kwa sheria ya ugavi wa mapato itacheleweshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *