Viwanja vitatu vimekamilika ,miaka miwili kabla ya kipute cha kombe la dunia 2022 Qatar

Ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya kung’oa nanga kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar tayari ujenzi wa viwanja vitatu umekamilika huku vikifanyiwa majiribio wakati vingine vikiendelea kujengwa.

Ukarabati wa miundo msingi umefikia asilimia 90 kukamilika ikiwemo viwanja vitatu vilivyo tayari kwa  matumizi vikiwa  Khalifa Internationa,Al Janooub na ule wa Education City na tayari Zaidi ya mechi 100 za majaribio zimeandaliwa katika viwanja hivyo mwaka huu .

uwanja wa Khalifa International
uwanja wa Al Janoub
Uga wa Education City

Nyuga nyingine tatu  zimo katika hatua za mwisho za ujenzi zikiwa ni pamoja na Al Rayyan,Al Bayt na Al Thumama wakati kazi ya ujenzi katika viwanja vingine viwili vya  Ras Abu Aboud ba Lusail vikitarajiwa kukamilishwa  mwaka ujao.

Uchanjaa wa Ras Abou
uga wa Al Rayan
uga wa Al Bayt
uwanja wa Al Thumama
Uwanja wa Lusail

Kinyume na Makala yaliyotangulia ya kombe la dunia mashabiki watakuwa na fursa ya kuhudhuria Zaidi ya mechi moja kwa siku wakati wa mechi za makundi  ambapo michuano minne itachezwa kila siku.

Viwanja vyote  vinane  vitakavyotumika kuandaa kipute cha kombe la dunia mwaka 2022 vitaunganishwa na na usfairi wa kisasa kumaanisha kuwa mashabiki ,maafisa na wanahabri watakuwa nan uwezo wa kusafiri kwa kutimia muda mfupi Zaidi kutoka uwanja mmoja hadi mwingine .

Uwanja wa  Al Bayt na ule wa Al Janoub ndivyo vilivyo mbali zaidi vikiwa umbali wa kilomita 75 baina yao .

Al Bayt Stadium, ulio na uwezo wa kuselehi mashabiki 60,000  ndio utaandaa sherehe za ufunguzi na pia mechi ya ufunguzi  wakati ule  wa Lusail unaomudu mashabiki 80,000  ukiandaa fainali Desemba 18 Mwaka  .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *