Vituo Vinane vya kuuza Petroli vyafungwa kwa kukiuka kanuni za mafuta

Halmashauri ya kudhibiti kawi na mafuta  (EPRA) imefunga vituo vinane vya petroli kwa kukiuka kanuni za mafuta za kuchanganya mafuta katika soko la humu nchini kati ya mwezi Julai na Septemba mwaka huu.

Kwenye taarifa kwenye ukurasa wake wa twitter, halmashauri hiyo imesema jumla ya sampuli  5,646 za mafuta zilifanyiwa uchunguzi katika vituo vyote 1,314 vya mafuta.

Asilimia  99.30 ya vituo hivyo vya  mafuta vilibainika kuwa vimezingatia kanuni hizo.

Kati ya vituo hivyo vinane vya mafuta vilivyofungwa , vilwili viko katika kaunti ya Bungoma, huku Kisumu, Mombasa, Nairobi, Kisii, na  Nakuru zikishuhudia kufungwa kwa kituo kimoja kila moja.

Baadhi ya vituo hivyo vilikuwa vikiuza mafuta ya  petroli ya  Super yaliyochanganywa na mafuta taa huku vingine vikiuza mafuta ya petroli ya Super na mafutaa taa yaliyonuiwa kuuzwa katika nchi za kigeni.

Halmashauri hiyo imebuni rasimu ya kanuni za usimamizi wa kawi ya mwaka huu ili kuboresha huduma za kawi na uhifadhi katika taasisi za kiviwanda na  kibiashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *