Vituko vya Eric Omondi

Mchekeshaji Eric Omondi hivi maajuzi alichapisha picha ya umbo lake jipya baada ya kuzamia mazoezi kwa nia ya kujenga misuli. Awali Eric alikuwa mwenye umbo dogo bila misuli.

Picha hiyo yake ndiyo alitumia wakati wa kuzindua studio yake na alitishia wanaume kwamba wanastahili kuficha wapenzi wao asije akawanyanganya.

Tangu wakati huo wachekeshaji wenza na hata wanamuziki wamekuwa wakimtania na hata kujaribu kuonyesha misuli yao huku wakijipaka mafuta ya kupikia.

Terrence Creative alichapisha video akiwa bila shati huku akijipaka mafuta hayo na kukashifu Eric kwa kuwaringia na umbo ambalo amepata maajuzi nao wamekuwa nalo kwa miaka mingi.

Mpenzi wake anasikika akimwambia kwamba amemaliza mafuta ya kupikia.

Njugush, Crazy Kenar na Henry Desagu hawakusaazwa kwenye shindano hilo la misuli lenye vichekesho tele.

Eric Omondi aliweka video ya Desagu kwenye akaunti yake ya Instagram akimsihi ampigie simu. Desagu anashangaa ni kwa nini anamtafuta baada ya kugura kundi analoliita “Wakonde forever” au anataka kurudi kundini?

Mwanamuziki Khaligraph Jones au ukipenda Papa Jones anamuingilia Eric akisema hakuna lolote ambalo amefanya katika kujenga misuli ati sasa ndio amejiunga na kundi la wakonde na ikiwa yeye na wengine wanataka kujenga misuli watafute ushauri wake.

Eric anamjibu Khaligraph kwa kuchapisha picha zake za awali akiwa hana misuli na kuandika, “Kijana mdogo amekuja Nairobi Juzi, Anabishana na wazee, by the time am done with you utakua umerudi back to factory setting. Taka taka ya Ghasia”

Chini ya picha hizo Khalighraph anajibu, “Hahaha Fala wewe, Ile look nilikuja nayo Nairobi ndio sai We unavaa kama Sunday Best”

Haijulikani shindano hili la misuli litaishia wapi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *