Visa vipya 186 vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Visa 186 vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa  COVID-19 vimeripotiwa kutokana na sampuli 8,049 zilizopimwa katika muda wa saa  24.

Hii ni kulingana na taarifa iliyotolewa na waziri wa afya Mutahi Kagwe. Jumla ya visa vilivyothibitishwa sasa imefikia 99,630 huku jumla ya watu 1,142,543 wakiwa wamepimwa.

Kati ya visa hivyo vipya  158 ni wakenya huku 28 wakiwa raia wa kigeni . Watu 112 ni wa kike na  74 ni wa kiume.

Mwathiriwa wa umri mdogo zaidi ni mtoto wa miaka miwili na wa umri mkubwa zaidi ana miaka  85.

Waziri alisema  Nairobi inaendelea kuongoza kwa visa vipya 95, Mombasa visa 23, Busia 17, Kiambu, 10, Isiolo na Kwale visa sita kila moja huku  Nakuru na  Uasin Gishu zikinakili visa vitano kila moja.

Kaunti ya Taita Taveta visa vitatu, Kajiado, Kakamega, Machakos, na  Kisumu zimeripoti visa viwili kila moja.

Kilifi, Nandi, Nyamira, Makueni, Migori, na  Bungoma vimeripoti kisa kimoja kila moja.

Watu 75 wamepona kutokana na ugonjwa huo, ambapo 34 kati yao walikuwa wakihudumiwa nyumbani na  14 waliruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya. Jumla ya watu waliopona hadi sasa ni 82,729.

Kagwe alisema wagonjwa watatu wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha 1,739 jumla ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa Covid 19 hapa nchini.

Aidha wagonjwa  674 wa COVID -19 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini na 1,543 wako chini ya mpango wa kuwahudumia waathiriwa wa Covid 19 nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *