Visa vipya 1,030 vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Nchi hii imenakili visa vipya 1,030 vya maambukizi ya Covid-19,kutokana na sampuli 8,316 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kiwango hiki cha maambukizi kwa mujibu wa wizara ya afya ni asilimia 12.4.

Idadi jumla ya visa vya maambukizi ya ugonjwa huo humu nchini sasa, imefikia 145,184.

Kati ya visa hivi vipya, 995 ni vya raia wa wakenya ilhali visa 35 ni vya raia wa kigeni.

Nairobi ingali inaongoza kwa visa 401 ikifuatiwa na Nakuru kwa visa 68,Kiambu 64,Kakamega 53, Machakos 51 Mombasa 51, na Uasin Gishu 44.

Wagonjwa 422 wamepona ugonjwa huo, 105 kutoka hospitali za humu nchini ilhali 317 ni kutoka ule mpango wa kuhudumiwa nyumbani.

Jumla ya wagonjwa waliopona sasa ni 98,605.

Kwa sasa kuna wagonjwa 1,616 waliolazwa katika hospitali mbali kote nchini, ilhali 4,243 wako chini ya mpango wa kuhudumiwa nyumbani.

Vifo 21 zaidiĀ  vimeripotiwa humu nchini kutokana na matatizo ya kiafya yanayosababishwa na ugonjwa wa COVID-19.

Kati ya visa hivi, wizara ya afya inasema visa vitano vilijiri katika muda wa mwezi mmoja uliopita ilhali vifo 16 vikiwa vile vilivyoripotiwa kuchelewa baada ya kutokea tarehe tofauti.

Wagonjwa 247 wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi,46 kati yao wakiwekewa vipumulio na wengie 170 wakipkea oksijeni ya ziada.

Wagonjwa 31 wanafanyiwa uchunguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *