Visa 991 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Wizara ya afya imesema kuwa watu 991 zaidi wameambukizwa virusi vya Covid-19, kutokana na sambuli 6,417 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kulingana na wizara hiyo, hiki ni kiwango cha asilimia 15.4  cha maambukizi ya Covid-19 hapa nchini.

Idadi jumla ya maambukizi nchini sasa ni 147,147 kutoka sampuli 1,571,244 zilizopimwa tangu mwezi Machi mwaka jana.

Kati ya visa hivyo vipya, 956 ni raia wa Kenya ilhali ilhali 35 ni raia wa kigeni ambapo 543 ni wa kiume na 448 ni wa kike.

Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miezi saba na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 99.

Watu 370 wamepona kutokana na ugonjwa huo, ambao 214 kati yao ni wale waliokuwa wakipokea matibabu nyumbani huku 156 wakiruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali mbali mbali kote nchini.

Idadi ya jumla ya waliopona kufikia sasa ni watu 99,580.

Jumla ya wagonjwa 1,607 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku wengine 5,996 wakihudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 239 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, ambapo 47 Kati yao wanatumia vipumulio na 161 wakipokea hewa ya ziada ya Oxygen. Wagonjwa 31 wangali wanafanyiwa uchunguzi.

Vifo 26 kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID – 19 vimeripotiwa na wizara ya afya katika muda wa mwezi moja uliopita.

Idadi hiyo sasa inafikisha 2,394 watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo nchini.

Wakati uo huo,wizara hiyo imetangaza kwamba kufikia siku ya Jumatatu, watu 526,026 wamepokea chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Kutoka idadi hiyo, 122,984 ni wahudumu wa afya, 42,343 ni maafisa wa usalama, 76,753 ni waalimu, huku 283,946 wakiwa raia wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *