Visa 633 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Taifa hili limenakili visa 633 vipya baada ya kupimwa kwa sampuli 5,193 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya visa vya Covid-19 hapa nchini sasa ni 108,362 kutoka kwa idadi jumla ya sampuli 1,327,999 zilizofanyiwa uchunguzi hapa nchini tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza mwezi machi mwaka jana.

Kati ya visa hivyo vipa 554 ni raia wa kenya ilhali 79 ni raia wa kigeni ambapo mwathiriwa mchanga zaidi ana umri wa mwaka mmoja na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 85.

kulingana na taarifa kutoka kwa wizara ya afya 384 ni wa kiume na 249 ni wa kike.

Wakati huo huo wagonjwa 374 wamepona virusi hivyo ambapo 328 walikuwa wakiuguzwa nyumbani na 46 waliruhusiwa kuondoka katika hospitali mbali mbali kote nchini. Idadi jumla ya waliopona virusi hivyo hapa nchini sasa 87,550.

La kuhuzunisha ni kwamba mtu mmoja amefariki kutokana na makali ya covid-19 na kufikisha idadi jumla ya waliofariki humu nchini kutokana na virusi hivyo kuwa 1,874.

Wagonjwa 483 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini huku wengine 1,389 wakiwekwa katika mpago wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani.

Kulingana na wizara ya afya wagonjwa 69 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo 26 wanatumia vipumulio na 33 wakipokea hewa ya oxygen ya ziada. Wagonjwa 10 wangali wanafanyiwa uchunguzi.

Kaunti ya Nairobi ilinakili visa 430, Kiambu visa 58, Kajiado 19 huku Migori na Uasin Gishu zikinakili visa 14 kila moja.

Kaunti ya Mombasa na Machakos ziliandikisha visa 7 kila moja. Trans Nzoia ilikuwa na visa 5, Kisumu 4 huku Kilifi,Kakamega na Makueni zikiwa na visa 3 kilamoja.

Bungoma,Kitui,Nyandarua na Narok zilinakili visa viwili kila moja. Kaunti ya Nyeri,Siaya,Taita Taveta,Turkana,Homa Bay,Laikipia,Lamu Meru Murang’a,Kericho na Kisii zikiandikia kisa kimoja kila kaunti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *