Visa 404 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Taifa hili limenakili visa 404 vipya vya Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 4,878 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya maambukizi ya Covid-19 hapa nchini sasa ni 92,459 huku idadi jumla ya sampuli zilizochunguzwa nchini hadi sasa ikiwa 987,683.

Kati ya visa hivyo vipya 364 ni wakenya ilhali 40 ni raia wa kigeni.

Aliye na umri mdogo zaidi ni mtoto wa miezi minane huku mwenye umri mkubwa zaidi ana miaka 79.

Wakati huo huo wagonjwa 527 zaidi wamepona virusi hivyo, 408 kutoka mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani huku 119 wakiruhusiwa kuondoka kutoka vituo mbali mbali vya afya.

La kuhuzunisha ni kwamba wagonjwa 11 zaidi wamefariki kutokana na makali ya covid-19 na kufikisha idadi jumla ya waliofariki nchini 1,604.

Kufikia sasa wagonjwa 871 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini huku 6,284 waki katika mpango wa utunzi wa nyumbani.

Wagonjwa 46 wako katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, ambapo 23 kati yao wanatumia vipumulio.

Wagonjwa wengine 46 wanatumia hewa ya ziada, 35 kati yao wakiwa katika wodi za kawaida na 11 wakiwa vituo vya HDU.

Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa maambukizi mapya ya virusi hivyo, huku ikinakili visa 118 ikifuatwa na kaunti ya kilifi kwa visa 110. Mombasa iliandikisha visa 66 vipya huku kaunti ya Makueni ikisajili visa 26 vipya.

Kaunti ya Nakuru ilinakili visa 23,Kiambu 12,Kisumu 11,Turkana 9 huku Kwale na Nyeri zikiwa na visa 5 kila moja.

Siaya na Kajiado zilinakili visa 4 kila moja, Murang’a 3, Machakos 2 huku Meru,Kakamega,Kericho,Kirinyaga,Marsabit na Lamu zikiwa na kisa kimoja kila moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *