Visa 325 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Taifa hili limenakili visa 325 vipya vya covid-19 baada ya kuchunguzwa kwa sampuli 3,282 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hii inaaashiria kiwango cha maambukizi cha  asilimia 9.9.

Idadi jumla ya maambukizi ya visa vya Covid-19 hapa nchini sasa  105,973. Kati ya visa hivyo vipya, 296 ni Wakenya na 29 ni raia wa kigeni.

Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa mwaka mmoja huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 85.

Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa kunakili visa  207 ikifuatwa na Busia kwa visa 30  nayo kaunti ya Mombasa ikaandikiaha visa 21.

Wakati huo huo wagonjwa 69 wamepona virusi hivyo ambapo 58 walikuwa wakiuguzwa nyumbani na 11 waliruhusiwa kuondoka katika hospitali mbali mbali humu nchini.

Idadi jumla ya waliopona corona humu nchini sasa ni  86,678.

Hata hivyo watu wawili wamefariki kutokana na makali ya virusi hivyo na kufikishwa Idadi jumla ya walioaga dunia hapa nchini kutokana na covid-19 kuwa 1,856.

Kwa sasa wagonjwa  347 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini huku wagonjwa1,495 wakihudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 58 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo 26 Kati yao wakitumia vipumulio na 28 wakipokea hewa ya ziada ya oxygen.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *