Visa 1,523 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Nchi hii imenakili visa 1,523 zaidi vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hii ni baada ya kupimwa sampuli 7,423 huku jumla ya visa vilivyothibitishwa humu nchini sasa ikifikia 141,365. Kiwango hiki cha maambukizi ni asilimia 20.5.

kati ya visa hivi vipya 1,432 ni vya Wakenya na 91 ni vya raia wa kigeni. Waathiriwa 681 ni wanawake na 842 ni wanaume.

Mgonjwa mchanga zaidi ni mtoto wa miezi mitatu na yule mkongwe zaidi ana umri wa miaka 105.

Nairobi ingali inaongoza kwa visa 626 ikifuatiwa na Kiambu kwa visa 142 na uasin Gishu kwa visa 108.

Hata hivyo wagonjwa 18zaidiĀ  wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa 2,276.

Wagonjwa 616 wamepona ugonjwa huo, 522 kutoka mpango wa kuhudumiwa nyumbani na 94 kutoka hospitali mbali mbali. Jumla ya wagonjwa walioponasasa imefikia 97,194.

Kwa sasa wagonjwa 1,591 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini ilhali wagonjwa 6,112 wako chini ya mpango wa kuhudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 236 wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi, ambapo 53 wanatumia vipumulio na 150 wanatumia oksijeni ya ziada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *