Visa 1,211 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Watu 1,211 wamebainishwa kuambukizwa virusi vya korona, kutoka kwa sampuli 9,304 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Idadi hiyo inafikisha  idadi jumla ya maambukizi hapa nchini ya Covid-19 hadi 76,404, tangu kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza mwezi machi mwaka huu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo, pia imeongezeka hadi 1,366 baada ya wagonjwa 17 zaidi kuaga dunia .

Hata hivyo wagonjwa 368 wamepona, 265 kati yao chini ya mpango wa uuguzi wa nyumbani,huku 103 wakiruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya .

Hadi sasa jumla ya wagonjwa 51,352 wamepona virusi hivyo hatari.

Wagonjwa wengine 1,134 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya ,67 kati yao wamelazwa katika vyumba vya matibabu maalumu ,huku 36 wakiwa kwenye vipumuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *