Vipusa wa soka kutoka Chile na China wafuzu kwa michezo ya Olimpiki

Timu za Chile na China zilijikatia tiketi kwa michezo ya Olimpiki mjini Tokyo Japan baada ya kusajili ushindi Jumanne usiku.

Chile ilifuzu kwa Olimpiki kwa mara ya kwanza baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Cameroon mjini Antalya , kwenye mchuano wa marudio  Jumanne usiku ,baada ya warembo hao wa Amerika Kusini kushinda mkondo wa kwanza mabao 2-1.

Kushindwa kwa Cameroon kulihuuisha matumaini ya Afrika kuwa na timu mbili mjini Tokyo na kuwaacha Zambia kuwa waakilishi pekee kutoka bara hili.

Katika mechi nyingine wasichana wa China walifuzu kwa makala ya 32 ya Olimpiki kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 4-3 ,licha ya kutoka sare ya 2-2 katika mkumbo wa pili Jumanne usiku ,baada ya China kushinda mkondo wa kwanza wa mchujo huo wa bara Asia 2-1.

China watakuwa wakishiriki Olimpiki kwa mara ya pili mtawalia baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro Brazil.

Mataifa yatakayoshiriki soka ya olimpiki mwaka huu ni :_wenyeji Japan,Uingereza,Uholanzi na Uswidi kutoka bara ulaya,Newzealand kutoka Oceania,Zambia ya Afrika,Australia na China kutoka Asia,Brazil na Chile kutoka Amerika kusini,Canada na USA za Amerika Kaskazini.

Timu zitakazocheza soka ya wanaume ni _;wenyeji Japan,Ufaransa, Ujerumani, Romania na Uhispania kutoka bara ulaya,Newzealand ya kutoka Oceania, wakati Afrika ikiwakilishwa na Cote d’Ivoire, Misri na Afrika Kusini.

Asia itakuwa na timu za Australia, Saudi Arabia, na  Korea Kusini ,Amerika Kusini itawakilishwa na Argentina na mabingwa watetezi Brazil wakati Amerika kaskazini na ya  kati wakiwa na  Honduras na  Mexico.

Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu itaandaliwa kati ya Julai 23 na Agosti 8 mwaka huu mjini Tokyo Japan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *