Categories
Habari

Viongozi wa jamii ya Pokot wataka kusitishwa kwa oparesheni ya kiusalama kapedo

Viongozi na watu wa jamii ya Pokot wameihimiza serikali kusitisha opareseheni ya kiusalama inayoendelea katika eneo la Kapedo,karibu na mpaka kati ya kaunti za Baringo na Turkana, ili kutoa fursa ya kufanywa mashauriano.

Wakiongozwa na gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo,viongozi hao waliihimiza serikali kuandaa mikutano ya amani na jamii za sehemu hiyo, kutafuta suluhisho la kudumu katika tatizo la utovu wa usalama katika sehemu hiyo.

Viongozi hao ambao walishutumu mauaji ya afisa wa GSU wa cheo cha juu siku ya jumapili katika eneo la Kapedo,waliazimia kushauriana na kushirikiana na idara za usalama ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Wakiongea mjini Makutano,viongozi hao walisema serikali inapaswa kutumia njia ya mashauriano kutatua tatizo la ujambazi katika sehemu hiyo.

Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing aliwakosoa viongozi wanaotoa matamshi ya uchochezi,lakini akawataka maafisa wa usalama  kutekeleza msako kwa njia ya utu.

Alitoa wito kwa serikali kuwasaka wahalifu na sio kulenga jamii yoyote.

Mbunge wa Kacheliba  Mark Lomunokol alitoa wito kwa serikali ya taifa kukumbatia mashauriano na kushirikiana na viongozi waKaunti ya Baringo hasaa kaunti ndogo ya Tiaty wanapotekeleza oparesheni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *