Vikosi vya Ulinzi humu nchini KDF vyasifiwa kwa juhudi za kupambana na ugaidi

Serikali imevihakikishia vikosi vya ulinzi vya humu nchini KDF kwamba inaviunga mkono katika juhudi zake za kukabiliana na ugaidi katika kanda hii.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya tisa ya siku ya vikosi vya ulinzi vya Kenya yaliyofanyika huko katika Kambi ya Jeshi ya Mariakani Kaunti ya Kilifi, Maziri wa Ulinzi Monica Juma amekariri mchango wa wanajeshi wa humu nchini katika kuleta uthabiti kwenye kanda hii na kimataifa.

Juma amesema kuwa serikali itaimarisha juhudi zake mara dufu kaitka kuhakikisha vikosi hivyo vina vifaa vyote vinavyohitajika katika kutekeleza jukumu lake la ulinzi.

Siku ya vikosi vya ulinzi vya Kenya huadhimishwa kila mwaka kwa heshima ya wanajeshi ambao hujitoa mhanga kulinda nchi.  

Hafla hiyo ya leo imetumiwa kudhihirisha umoja na familia za wanajeshi wa sasa na wale wa zamani ambao wangali wanaponya majeraha na kiwewe kinachotokana na majukumu yao.

Tangu vikosi vya ulinzi vya Kenya vilipojiunga na ujumbe wa muungano wa Afrika nchini Somalia, vimepiga hatua kubwa katika kukabiliana na shughuli za kigaidi kwenye kanda hii.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *