Vijana kaunti ya Kwale waonywa dhidi ya kuingizwa katika itikadi kali

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya ametoa wito kwa vijana wa kiislamu kukataa kuingizwa katika itikadi kali za kidini na kudumisha amani, umoja na uvumilivu.

Alitoa wito kwa vijana kukataa maovu kama vile itikadi kali, uhalifu, matumizi ya dawa za kulevya na kujiepusha na vitendo vyovyote ambavyo huenda vikahatarisha maisha yao ya siku za usoni.

Gavana  Mvurya alisema kuwa dini ya kiislamu inahimiza amani na umoja na kuwa itikadi kali na ghasia hazina nafasi katika jamii.

Mvurya alikuwa akiongea katika afisi yake mjini Kwale ambapo alimpokea Yunus Masoud mwenye umri wa miaka  15, ambaye alikuwa mshindi wa shindano la kila mwaka la Quran lililoandaliwa nchini  Tanzania.

Mvurya alisema kuwa wazazi wanapaswa kuwahimiza watoto wao kudumisha maadili na kuimarika katika maswala ya ya elimu ya kidunia na kidini.

Alisema kuwa kuwahimiza watoto kudumisha maadili kutasaidia kuzuia maaovu kama imani katika itikadi kali na matumizi ya dawa za kulevya.

Alitoa wito kwa waislamu kuzingatia haki wakati huu wote wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *