Vihiga United waipiga kumbo Kisumu All Stars na kurejea ligi kuu FKF

Timu ya Vihiga United Fc imerejea katika ligi kuu ya FKF baada ya washinda Kisumu All Stars mabao 5-3 kupitia mikwaju ya penati katika mechi ya marudio iliyochezwa Jumatano alasiri katika uwanja wa Moi,kaunti ya Kisumu.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     Vihiga iliyokuwa imepoteza mabao 1-2 nyumbani Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Mumias sports Complex,ilijikuta taabani  baada ya  Eric Otieno  kuwafungia All Stars  kabla ya

Dennis Wafula kusawazisha kwa Vihiga huku kipindi cha kwanza kikimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Hata hivyo matumaini ya All Stars kusalia ligini yaliyeyushwa baada ya beki wao Jeckoniah Ogendo kuunawa mpira na kuwazawadi wageni penati iliyofungwa na Patrick Okulo katika dakika ya 55.

Pambano hilo lilimalizika kwa sare ya 3-3 na ikabidi kuamuliwa kupitia penati huku Vihiga wakirejea ligini kwa mara ya pili tangu washushwe ngazi mwishoni mwa mwaka 2018.

Kisumu All stars watalazimika kucheza ligi ya kitaifa Supa kuwania fursa ya kurejea tena ligini .

Mchujo huo huwashirikisha wanaomaliza katika nafasi ya tatu katika ligi ya Nsl na timu nambari 16 katika ligi kuu.

Vihiga United inajiunga na mabingwa wa Nsl Nairobi City Stars na Bidco United kushiriki ligi kuu ya FKF kuanzia Novemba 20.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *