Vigogo walamba sakafu katika uchaguzi wa FKF

Viroja kadhaa vilishuhudiwa katika uchaguzi wa shirikisho la soka nchini Fkf kiwango cha kaunti ulioanndaliwa jumamosi Septemba 19 .

Zoezi hilo lilifanyaika katika kaunti 21  kote nchini huku baadhi ya vigogo na wandani wa karibu wa Rais wa sasa Nick Mwendwa wakitemwa nje.

Kulingana na mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi wa Fkf Bi Kentice Tikolo Zoezi hilo liliandaliwa kwa njia huru na wazi licha kuripotiwa kwa visa vichache vya hitilafu.

“Kura zimeenda vizuri vile tulipanga,ingawa tumekuwa na kasoro chache mfano Kisumu kulikuwa na kundi la vijana waliotaka kuingia katika eneo la kupigia kura kwa nguvu,Garisa pia uchaguzi ulisamamishwa baada ya mmoja wa waaniaji kupeleka kesi katika makahama kuu.kifupi  katika maeneo mengi uchaguzi umeandaliwa vyema” akasema tikolo akizungumza na Kbc radio Taifa kupitia simu

Mmoja wa wagombeaji katika kaunti ya Narok alidinda kupiga kura  huku ukifutiliwa mbali katika kaunti ya Garisa na sasa bodi ya uchaguzi itakuatana baade wiki hii kuamua hatima yake.

Wakili Amos  Otieno alimbwaga mwandani wa karibu wa Nick Mwendwa –George Onyango kwa kupata kura 51  dhidi ya 45 za Onyango  na kuchaguliwa mwenyekiti wa Fkf Nairobi East.

Onyango, alikuwa ameshinda katika chaguzi mbili zilizofutiliwa mbali na mahakama kabla  ya kuonyeshwa kivumbi jana.

Caleb Malweyi alijizolea kura 53 na kutwaa uenyekiti wa Nairobi West dhidi ya  Charles Njoroge aliyepata kura tatu .

mmoja wa wapiga kura kwenye kituo cha Nairobi

Luthers Mokua aliyekuwa afisa mkuu mtandaji wa timu ya Wazito Fc ndiye mwenyekiti wa Fkf tawi la Nyamira alipopata kura 14 dhidi ya Thomas Mayaka aliyekuwa na kura 1.

Peter Karino aliteauliwa bila upinzani katika kaunti ya Narok baada ya mpinzani wake Naftali Kirui kujiondoa kwa madai ya  udanganyifu.

Chrispine Ochieng ndiye mwenyekiti wa Nyeri huku mwanasoka wa zamani  Dickson Oruko akishinda kiti hicho katika kaunti ya Kisumu.

Kule Mombasa  Alamin Abdalla  alimshinda  Lilian Nandundu  kwa kura 1 pekee alipopata kura 17 dhidi ya 16,na pia Abdala alikuwa ameshindwa na Nandundu kwenye chaguzi mbili zilizofutiliwa mbali.

Hatimaye kutoka  Busia, Hillary Musundi alichaguliwa mwenyekiti  mpya.

Maafisa wa kaunti waliochaguliwa jana watahudumu kwa kipindi cha miaka minne na watapiga kura kuwachagua maafisa wa kitaifa tarehe 17 mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *