Vifo 26 zaidi vyaripotiwa Kenya kutokana na maradhi ya COVID-19

Nchi hii imenakili vifo 26 zaidi vilivyotokana na virusi vya korona na kuifanya idadi jumla ya maafa hayo kufikia 2,420.

Aidha, watu 981 wamethibitishwa  kuwa na virusi hivyo baada ya kupimwa kwa sampuli 7,529 katika muda was aa 24 zilizopita, takwimu zinazowakilisha asilimia 13 ya maambukizi hayo.

Takwimu hizo zimefikisha idadi jumla ya maambukizi nchini kuwa watu 148,128 na ile ya sampuli zilizopimwa kuwa 1,578,773 tangu mwezi Machi mwaka wa 2020.

Kati ya visa hivyo, watu 961 walikuwa Wakenya huku 20 wakiwa raia wa kigeni. Wagonjwa 563 walikuwa wanaume huku 418 wakiwa wanawake.

Mgonjwa mchanga zaidi alikuwa mtoto wa siku saba huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 97.

Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza baada ya kunakili visa 349, ikifuatwa na Bungoma kwa visa 61, Turkana 55, Kiambu 49, Kisumu 46, Mombasa 46, Nakuru 41, Uasin Gishu 39, Meru 35, Busia 24, Kajiado 23, Siaya 20, Kilifi 19, Migori 17, Taita Taveta 17, Kitui 16, Kakamega 12, Machakos 12, Isiolo 11, Nandi 13, Nyandarua 10, Vihiga 9, Kirinyaga 8, Homabay 7, Kericho 7, Murang’a 6, Kisii 5, Laikipia 5, Makueni 5, Marsabit 4, Nyeri 3, West Pokot 3, Baringo 1, Kwale 1, Samburu 1 na Trans Nzoia 1.

Wakati uo huo, wagonjwa 665 wamepona huku 528 wakitoka katika mpango wa kutibiwa nyumbani na 137 wakitoka katika hospitali mbali mbali nchini, hivyo jumla ya waliopona ikafika 100,245.

Kufikia sasa wagonjwa 1,623 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini, huku wengine 5,565 wakiwa wanahudumiwa nyumbani.

269 kati ya walio hospitalini wako kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi, 47 wakiwa wanatumia vipumulio na 172 wakipokea hewa ya ziada ya oksijeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *