uwanja Nyayo kufunguliwa rasmi Jumamosi

Uwanja wa taifa wa Nyayo utafunguliwa rasmi jumamosi hii Septemba 26 , ili kuanza kutumika kwa shughuli za michezo, ikiwa wiki moja tu kabla ya mashindnao ya riadha ya Kip Keino Classic Continental tour kufanyika katika uga huo.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza ufunguzi wa uwanja huo jumamosi hii ,hafla inayotarajiwa kuhudhuria na wadau mbalimbali kutoka sekta ya michezo nchini Kenya.

Uwanja huo umekuwa ukifanyiwa ukarabati kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita wakati  Kenya ilipokezwa maandalizi ya mashindnao ya kombe la Chan huku shughuli za ujenzi zikikwama kwa wakati Fulani.

Sehemu ya uwanja wa Nyayo iliyokarabatiwa

Uchanjaa wa Nyayo ulijengwa na marehemu rais Daniel Moi mapema miaka ya 80 na kuandaa makala ya 4 ya mashindano ya All Africa games mwaka 1987.

Uga huo unaomudu mashabiki  30,000  pia ulitumika kuandaa mashindnao ya riadha ya Afrika mwaka 2010 huku mibabe kama vile Amantle Montsho wa Botswana ,Blessings Okagbare kutoka Nigeria , Tirunesh Dibaba wa Ethiopia wakishiriki na  David Rudisha wa humu nchini.

Uwanja wa Nyayo baada ya ukarabati

Baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa Ukarabati ni jukwaa kuu,vyumba vya kubadilisha mavazi,Vyoo,kidimbwi cha kuogelea ,zulia ya kukimbilia na  viti.

Mara ya mwisho kwa uwanja huo kuandaa michezo ilikuwa tarehe 8 mwezi Machi mwaka huu yakiwa makala ya 5 ya mbio za Beyon Zero Half Marathon ,hafla ambayo pia ilihudhururiwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Mashindano ya continental tour yatakuwa katika vitengo vya Discretionary Events Javelin,mita 5000,mita 1500,Mita 800 na mita 400 wanaume kwa wanawake na mashindano ya kitaifa yatakayojumuisha fani za 20 Km Walk ,High Jump ,Long Jump ,4 X 400m Mixed ,mita 10000 na 400M Hurdles.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *