Usimamizi mbaya wa FKF walaumiwa kwa kudorora kwa soka ya Kenya

Kocha wa Kenya mwenye makaazi yake nchini Marekani Goerge Achar ameshutumu usimamizi wa sasa wa FKF kwa kukuosa  kuleta utaalamu wa kisasa  na ufundi unaohitajika  ili kuinua viwango vya mchezo wa soka nchini .

Achar ametaja mvutano unaoshuhudiwa kuhusu mkataba wa FKF na kampuni ya Star Times  ambapo timu 4 zilidinda kusaini mkataba na kupelekea Mathare United na Zoo fc kupigwa marufuku ,kuwa  ishara ya uongozi mbaya na badala yake shirkisho lapaswa kujadiliana na vilabu husika na kuafikia mwafaka.

“Tunakosa uongozi wa utalaam  ,tunao viongozi ambao hawana mapenzi ya soka  ,wanajidai wanapenda mchezo wa soka lakini tabia zao zinaashiria kinyume ,tunao wachezaji wengi wenye vipaji lakini kukosena kwa uongozi bora na usimamizi mzuri umechangia wengi wao kutofikia viwango vyao vya juu katika mchezo”.

“Tabia za kusimamia soka kwa majigambo na kujipiga kifua hakutapeleka mchezo wetu mahali popote .FKF inapaswa kuwasikiza wadau ,vilabu na kufanya nao kazi kwa pamoja badala ya kuwapiga vita na kuwaadhibu,pia FKF inapaswa kuwaajiri wataalam kusimamia idara mbali mbali  za shirikisho”akasema Achar

Achar, ambaye pia anamiliki wakfu wa  Sophie George Foundation  unaoandaa kliniki za soka kwa wachezaji chipukizi katika maeneo mbalimbali nchini , amesema kuwa shughuli zao ziliathirika pakubwa kutokana na janga la COVID9 19 lakini wanatarajia kurejelea hali ya kawaida mwaka ujao wakilenga kuwakuza wanasoka chipukizi kutoka familia maskini.

“Tumelazimishwa kupunguza shughuli zetu mwaka huu kutokana  na janga la Covid 19 ,tulipanga kuandaa kliniki Ruiru na Nakuru  jambo ambalo halikuwezekana .Katika juhudi zetu tumekuza na kulea vipaji vingi wakiwmeo  kapteni wa zamani wa Harambee Stars Robert Mambo na Hussein Mohammed wa Ulinzi Stars ,na kwenda mbele kuna matumaini ya kufanya makubwa” akakariri Achar

Kocha Achar na wenzake wakitoa mafunzo ya soka kwa Vijana

Achar ameitaka FKF kuongeza juhudi katika kituo cha kitaifa  cha kukuza talanta kilichozinduliwa mwaka 2019 ili kuhakisha kituo hicho kinatoa wachezaji wanaojiunga na timu za taifa katika viwango vyote kila wakati.

“Huku ni kujidanganya kwamba tunajenga timu ya taifa,hakuna vile tutachukulia kuwa wavulana walio katika kituo hicho  ndio bora zaidi bila kushirikisha wachezaji walio katika matawi yote ya vituo hivyo nchini kushindana kikamilifukabla ya wale bora kuchaguliwa mwishoni mwa mwaka na kujiunga na timu za taifa “akaongeza Achar

Kocha Achar akitoa mafunzo katika mojawpao wa kliniki

Achar anayeishi Marekani kwa sasa anaifunza timu ya chipukizi walio chini ya umri wa miaka 16 ya La Mexicana katika jimbo la Dallas na akicheza soka nchini alikuwa na timu za   Lake Warriors FC na FC Ramogi katika ligi kuu ya Kenya miaka 80, kabla ya kuhamia Marekani ambako pia aliichezea timu ya  FC Dallas.

Mahakama ya SDT  Ijumaa iliyopita  iliamuru FKF kuziruhusu timu za Mathare United na Zoo Fc ambazo zilikuwa zimepigwa marufuku kucheza ligi hiyo ,huku uamuzi kuhusu kesi iliyo mbele ya mahakama hiyo ukisubiriwa.

FKF imezishurutisha timu zote zinazoshiriki ligi kuu msimu huu kusaini mkataba wa Stars Times kabla ya kukubaliwa kucheza ligi kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *