Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Malindi kugharimu shilingi bilioni 4.3
Halmashauri ya viwanja vya ndege inataka shilingi bilioni 4.3 ili kununua kipande cha ardhi kwa upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Malindi katika kaunti ya Kilifi.
Mkurugenzi wa uwanja huo Ramadhan Karama ametoa wito kwa bunge la kitaifa kuingilia kati ili kuharakisha kutolewa kwa fedha hizo.
Amesema fedha hizo zinahitajika ili kuwafidia maskwota na kutoa nafazi kwa hawamu ya pili ya upanuzi wa uwanja huo.
Akiongea kwenye uwanja huo wa ndege wakati alipoalika kamati ya bunge kuhusu uchukuzi, Karama amesema kuendelea kucheleweshwa kwa fedha hizo unakokota upanuzi wa uwanja huo.
Karama amesema dhamani ya shamba katika eneo hilo inaendelea kupanda na huenda ikagharimu pesa nyingi zaidi siku zijazo.
Halmashauri ya viwanja vya ndege inanuia kuongeza urefu wa barabara ya kutua ndege hadi urefu wa kilomita 2.4 ili kutoa nafazi ya kutua kwa ndege kubwa.