Ujenzi wa jiji la konza warejelewa baada ya kudumazwa na janga la Covid-19

Shughuli za ujenzi katika jiji la  Konza Technopolis zimeanza baada ya kusimamishwa kwa muda kutokana na vikwazo vya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa covid-19.  

Afisa mkuu mtendaji wa Konza Technopolis John Tanui amesema wanakandarasi sasa wanafanya kazi saa 24 kwa siku huku zaidi ya wafanyakazi  1000 wakiwa katika eneo hilo ili kuokoa muda uliopotezwa.

Mji huo unatarajiwa kusuluhisha tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini lililozidishwa na janga la viris vya corona.

Kamati ya bunge la taifa kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano ikiongozwa na mwenyekiti wake William Kipkemoi Kisang, imesema itatoa usaidizi wa kutosha kwenye bajeti kwa mradi huo kutokana na manufaa yake makubwa ya kiuchumi yanayotarajiwa sio tu kwa nchi hii bali pia kwa bara zima la Afrika.

“ Tumewekeza zaidi ya shilingi bilioni 100 na hii ni hakikisho kuwa serikali imechukulia mradi huu kwa uzito zaidi na tutaendelea kutenga fedha kuona kwamba maono ya kuwa na mji huu yanaafikiwa,” alisema Kipkemoi

Kisang amesema kupitia mashauriano ya idara mbali mbali, serikali itaharakisha ujenzi wa bwawa la maji la Thwake ili kuhakikisha jiji la  Konza linapata maji ya kutosha yanayohitajika kwa ukuaji wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *