Uingereza yaruhusu tena mashabiki viwanjani

Baada ya subira ya miezi 8  ,hatimaye mashabiki watarejea uwanjani Emirates Alhamisi usiku kushuhudia mechi ya raundi ya tano ya Europa League kati ya Arsenal dhidi ya Rapid Vienna ya Austria.

Uingereza ilitangaza kurejea kwa mashabiki viwanjani kuanzia Disemba 2  mwaka huu, lakini kwa mechi zinazochezwa katika miji kadhaa huku miji mingine mashabiki wakisalia kupigwa marufuku.

Arsenal itakuwa kilabu ya kwanza inayopiga  ligi kuu Uingereza kuruhusiwa kuwa na mashabiki wasiozidi 2000 uwanjani watakapochuana na Rapid Vienna Alhamisi usiku.

Mashabiki walikuwa wamepigwa marufu kuingia viwanjani nchini Uingereza mwezi Machi huu kutokana na ugonjwa wa Covid 19,lakini makataa ya Lock Down yaliyowekwa na Waziri mkuu Boris Johnson yalikalimilika Disemba Mosi na hivyo mashabiki walianza kurejea kutazama mechi viwanjani katika baadhi ya miji ya Uingereza Disemba 2.

Hata hivyo idadi kubwa ya mashabiki wanaoruhusiwa kuingia uwanjani nchini Uingereza ni 4000  pekee kulingana na mji wa timu inayocheza nyumbani,.

Serikali ya Uingereza imeratibu miji yake kwa viwango vitatu ambapo timu zinazopatikana katika kiwango cha kwanza cha  miji  zitaruhisiwa kuwa na mashabiki 4000, timu kutoka viwango vya pili vya miji mashabiki 2000 wataruhusiwa huku timu kutoka viwango vya tatu vya miji vikipigwa marufuku kuwa na mashabiki viwanjani.

Sheria hiyo inaruhisiwa kwa mashabiki wa timu za nyumbani pekee.

Hatua hii ina maana kuwa timu zote za soka kutoka miji ya Manchester, Newcastle, Sheffield, Wolverhampton Birmingham, Leicester na  Leeds ambayo yote imewekwa katika kiwango cha tatu hazitaruhusiwa kuwa na mashabiki viwanjani.

Timu zinazoruhisiwa kuwa na mashabiki wasiozidi 2000 ni za kutoka miji ya London, Liverpool, Southampton na  Brighton ,miji ikipangwa katika kiwango cha pili kumaanisha kuwa vilabu vitakavyokubiliwa kuwa na mashabiki  kwenye viwanja vya nyumbani  kaunzia Disemba 2 ni  Liverpool, Everton, Tottenham, Chelsea, West Ham, Crystal Palace, Arsenal, Fulham, Brighton na Southampton katika ligi kuu Uingereza huku vilabu vya  Aston Villa, Burnley, Leeds United, Leicester City, Manchester City, Manchester United, Newcastle United, Sheffield United, West Brom na  Wolves vikipigwa marufuku kuwaruhusu mashabiki viwanjani.

Ligi zote za Uingereza zikiwemo Premier League, Championship, League One, League Two, National League, National League South, National League North na ligi nyingine zote  za viwango vya chini ziko huru kuruhusu mashabiki kurejea viwanjani.

Pia shirikisho la soka ulaya UEFA litaruhusu mashabiki kuhudhuria mechi kwa kuzingatia sheria za taifa husika lakini hadi asilimia 30 pekee ya mashabiki watakubaliwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *