“Uhalifu na Haki”

Kazi ya kuunda kipindi kwa jina “Crime and Justice” imeanza na waigizaji maarufu nchini Kenya Sarah Hassan na Alfred Munyua ndio wahusika wakuu.

Kipindi hicho kinaundwa na kampuni ya mitandao ya kuuza vipindi kwa jina ‘Showmax’ na runinga ya ‘Canal+’ na kitahusu matukio ya kila siku.

Sarah Hassan ataigiza kama ‘Makena’ na Alfred Munyua aigize kama ‘Silas’ na kwa pamoja wanaigiza kama wapelelezi ambao wanafuatilia matukio mbali mbali ya uhalifu na kuhakikisha kwamba haki inatendeka.

Walipohojiwa, Sarah alikiri kwamba ndio mara ya kwanza anaigiza katika jukumu kama hilo la upelelezi na kwamba linampa nafasi ya kukua kama muigizaji.

Alfred naye anafurahia jinsi nafsi ya Silas inadhihirika kwenye mswada wa kipindi hicho. Kulingana naye jukumu lenyewe sio gumu na kwamba Silas hajaonyeshwa kama aliye na uwezo usio wa kawaida bali ni mtu wa kawaida ambaye anafanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha kesi zinatamatika na haki inatendeka.

Waigizaji wengine ambao wamehusishwa kwenye kipindi hicho ni pamoja na Maqbul Mohaamed ambaye ataigiza kama mkuu wa DCI kwa jina “Kebo”, Paul Ogola kama mwendesha mashtaka kwa jina “Sokoro” na Brian Ogola kama “Caleb” ambaye ni mchunguzi wa maiti na muigizaji wa muda mrefu John Sibi- Okumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *