Ugonjwa wa ajabu waripotiwa Tanzania ambapo waathiriwa wanatapika damu

Ugonjwa usiojulikana umeripotiwa na vyombo vya habari katika eneo la Kusini Mashariki mwa Tanzania, ambapo imesemekana waathiriwa wanatapika damu.

Maafisa wa afya katika Wilaya ya Chunya wamenukuliwa wakisema baadhi ya waathiriwa walifariki baada ya saa chache tu.

Mnamo tarehe 5 mwezi huu, Diwani wa Ifumbo wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya, Weston Mpyila, aliitaka serikali kuwasaidia kupata ufumbuzi kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huo, akidai zaidi ya watu 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 wakiambukizwa.

Wizara ya Afya ya nchi hiyo imesema ilituma kundi la watalamu kuchunguza ripoti hizo lakini wakasema hakuna chamuko lolote.

Hata hivyo, Waziri wa Afya wan chi hiyo Dorothy Gwajika amemsimamisha kazi afisa mkuu wa matibabu katika wilaya hiyo aliyenukuliwa akithibitisha ugonjwa huo.

Wizara hiyo imesema imebainisha kuwa dalili za ugonjwa huo zilianza kuripotiwa tangu mwaka wa 2018.

Imehimiza umma kudumisha utulivu huku ikichunguza na kuahidi kutoa habari kuhusu ugonjwa huo.

Raia wa Tanzania wamehimiza kuboresha kinga zao za mwili kwa kutumia dawa za miti shamba huku kukiwa na janga la ugonjwa wa COVID-19.

One thought on “Ugonjwa wa ajabu waripotiwa Tanzania ambapo waathiriwa wanatapika damu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *