Uganda na Tanzania zafuzu AFCON U 17 mwakani nchini Moroko

Uganda na Tanzania zimefuzu kwa kipute cha kombe la AFCON mwezi Juni mwaka ujao nchini Moroko, baada ya kujikatia tiketi kwa nusu fainali za kombe la CECAFA nchini Rwanda siku ya Jumapili.

Uganda walihitaji bao lake Oscar Mawa kuwabandua  Djibouti katika nusu fainali ya kwanza uwanjani Umuganda wilayani Rubavu, huku Tanzania maarufu kama Serengeti boys wakiishinda Ethiopia penati 4-3  kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Ni mara ya pili mtawalia  kwa timu za Uganda na Tanzania kufuzu kwa kipute cha AFCON kwa chipukizi baada ya timu zao kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 kufuzu maajuzi nchini Tanzania.

Fainali ya Jumanne ya Cecafa itatanguliwa na mchuano wa kuwania nafasi ya tatu na nne kati ya Ethiopia na Djibouti katika uga wa Umuganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *