Uganda Cranes yaikwaruza Zambia mechi ya kujinoa kwa CHAN

Uganda Cranes iliibwaga Chipopolo ya Zambaia mabao 2-0 Jumatatu jioni katika mechi ya pili ya mashindano ya kutangulia makala ya 6 ya michuano ya CHAN nchini Cameroon,mechi iliyosakatwa katika uwnaja wa Annex Omnisports mjini Younde.

Vianne Sekajugo na Steven Mukwala waliifungia Cranes mabao hayo katika dakika ya 25 na 60 mtawalia ,Waganda wakiendeleza msururu wa matokeo mazuri baada ya kwenda sare ya 1-1 na wenyeji Cameroon katika mechi ya kwanza ya  ya mashindano hayo yanayotangulia michuano ya CHAN.

Uganda watafungua ratiba ya kundi C katka makala ya 6 ya michuano ya Chan dhidi ya Amavubi ya Rwanda Tarehe 18 mwezi huu kabla ya kumenyana na Zimbabwe Januari 22 na kukamilisha ratiba dhidi ya Togo Januari 26.

Michuano ya Chan ambayo hushirikisha wachezaji wanaopiga soka katika ligi za nyumbani yataanza Januari 16 na kukamilika Februari 7 huku mataifa 16 yakiwania kombe hilo linaloshikiliwa na Moroko.

Runinga ya taifa KBC Channel 1   itakuletea mechi zote live kutoka Cameroon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *