Uchaguzi wa fkf kuendelea Jumamosi ilivyopangwa

Uchaguzi wa Fkf  ambao umekuwa ukisubiriwa kwa hamu na ghamu utaendelea Jumamosi ilivyopangwa katika mkahawa wa Safari Park.

Zoezi hilo litaendelea mbele ilivyopangwa baada ya bodi ya mahakama inayosikiza kesi za michezo chini ya uongozi wa Jaji John Ohaga kuamuru Ijumaa alasiri kuwa uchaguzi huo endelee mbele ilivyopangwa.

Kwenye uamuzi wake Ohaga ametupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Sam Nyamweya, Nicholas Musonye na  Twaha Mbarak,kupinga uhalali wa uchaguzi.

Wagombezi wane wanampinga kinara wa sasa Nick Mwendwa aliye na umri wa miaka 41 wakiwemo Herbert Mwachiro, Dan Mule, Lordvick  Aduda, na  Boniface Osano.

Kulingana na mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi Kentice Tikolo wamekamilisha matayarisho kwa uchaguzi huo wa  Jumamosi huku wakiwa tayari kuandaa uchaguzi huru na wa haki.

‘’tuko tayari kwa uchaguzi wa Jumamosi,na tutahakikisha utakuwa huru na haki’’akasema Bi Tikolo

Kwa mjibu wa Tikolo Wajumbe 87 kutoka kaunti zote 47 watapiga kura kesho huku mshindi wa Urais akihitaji asilimia 50 na kura mora moja ya kura zote katika raundi ya kwanza ,la sivyo basi wataingia awamu ya pili ya upigaji kura.

Wachunguzi kutoka Fifa wanatarajiwa kufuatilia uchaguzi kupitia mitandaoni kutoka Geneva Switzerland kulingana na Bi Tikolo.

Kando na wenyeviti wa kaunti kutakuwa na wapiga kura kutoka ligi kuu,National super league ,ligi kuu ya wanawake na vilabu kutoka division one.

Uchaguzi wa Fkf awali umefutiliwa mbali na mahakama ya kutatua migogoro michezoni mara mbili kwa kutozingatia sheria.

Watakaochaguliwa Jumamosi watahudumu afisini kwa miaka minne.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *