Uchaguzi wa Ann Wanjiku kibe kuwa mbunge wa Gatundu Kaskazini wafutiliwa mbali

Mahakama kuu imebatilisha kuchaguliwa kwa Ann Wanjiku Kibe kuwa mbunge wa Gatundu Kaskazini.

Akitoa uamuzi huo, jaji Weldon Korir alisema Wanjiku alichaguliwa kuwa mbunge kinyume cha sheria.

Mahakama ilielezwa kuwa alipochaguliwa kuwa mbunge mwaka 2017, Wanjiku alikuwa bado ni mwakilishi wa Wadi.

Jaji Korir pia alimuagiza naibu msajili wa mahakama kumjulisha spika wa bunge la kitaifa kuhusu uamuzi huo ili tume ya IEBC iweze kuandaa uchaguzi mpya.

Mnamo tarehe-25 mwezi Juni mwaka huu, mahakama ya rufani iliagiza rufaa ya kupinga kuchaguliwa kwa Ann Wanjiku isikilizwe upya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *