Trump na Mkewe wapatikana na Corona

Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 pamoja na mkewe Melania Trump.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 74 ameweka tangazo hilo kwenye mtandao wake wa Twitter.

“Usiku wa leo, @FLOTUS na mimi tumethibitishwa kuambukizwa COVID-19. Tutaanza mchakato wa kujitenga na kutibiwa upesi. Tutashida hili pamoja,” ameandika Trump.

Haya yanajiri muda mfupi baada ya mfanyikazi wa karibu wa rais huyo kuambukizwa ugonjwa huo.

Hope Hicks, mwenye umri wa miaka 31 na ambaye ni mshauri wa rais Trump ndiye mhudumu wake wa karibu zaidi aliyeambukizwa.

Trump na Hicks walisafiri pamoja kutumia ndege ya Air Force One hadi katika mahojiano katika kituo kimoja cha runinga mjini Ohio wiki hii.

Alhamisi, Trump alisema atajitenga pamoja na mkewe baada ya Hicks kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo.

Haijabainika kama kuambukizwa kwa Trump kutaathiri maandalizi ya mdahalo wa pili wa urais nchini humo uliopangwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu huko Miami, Florida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *