Trump ashinikiza kupunguzwa kwa ruzuku za walioathirika na COVID-19 Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amelitaka Bunge la Congress kuufanyia marekebisho mswada kuhusu ugonjwa wa COVID-19 ambao unalenga kutoa ruzuku ya dola 2,000 kwa kila raia nchini humo ili kujikinga na athari za janga hilo.

Kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Trump amewataka wabunge kupunguza pesa zinazotumika visivyo, huku akisema ni ubadhirifu unaoleta aibu.

Amesema kiwango cha dola bilioni 900 za Kimarekani ambazo zimejumuishwa kwenye mswada wa kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19, hazihusiani na janga hilo.

Mswada huo ulikusudia kuwapa raia wa Marekani wengi msaada wa dola 600 kufuatia janga hilo.

Siku ya Jumanne, Rais Mteule Joe Biden alisema kuwa kiasi hicho cha pesa ni kidogo na kwamba atashinikiza bunge kutenga fungu kubwa la fedha kuwasaidia walioathirika kutokana na janga la COVID-19 atakapoingia afisini rasmi mwezi Januari.

Trump, ambaye ataacha madaraka tarehe 20 mwezi Januari, anatarajiwa kutia saini mswada huo uwe sheria, licha ya kuonyesha kutoupendelea, akisema ni ufujaji wa pesa za Wamarekani ambao wanajikakamua kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *