Trump abadili mpango wa kutaka maafisa wa White House wawe wa kwanza kupokea chanjo ya COVID-19

Rais wa Mardekani Donald Trump amebadili mpango wake wa awali wa kutaka maafisa wa Ikulu ya White House kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Ilikuwa imetangazwa hapo awali kuwa maafisa wakuu kwenye utawala wa Trump watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupokea chanjo hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Pfizer/BioNTech.

Serikali ya Marekani imeidhinisha matumizi ya chanjo hiyo kuanzia hivi leo, inayosemekana inaweza kukinga asilimia 95 ya virusi vya Corona.

Dozi za kwanza milioni tatu za chanjo hiyo zimesambazwa katika majimbo yote 50 nchini Marekani.

Shehena ya kwanza ya chanjo hiyo iliondoka huko Michigan Jumapili huku wahudumu wa afya na wakongwe wakipewa kipaumbele katika utoaji wa chanjo hiyo.

Taarifa kwamba maafisa katika Ikulu ya White House watakuwa wa kwanza kupokea chanjo hiyo zilishtumiwa katika mitandao ya kijamii.

Vifo vilivyotokana na ugonjwa wa COVID-19 vimekuwa vikiongezeka maradufu nchini Marekani tangu mwezi Novemba huku idadi kubwa zaidi ya vifo 3, 309 ikiripotiwa siku ya Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *