Trippie Redd ajifananisha na Lil Wayne

Trippie Redd ambaye ni mwanamuziki wa mtindo wa rap nchini Marekani anasema yeye ndiye Lil Wayne wa sasa. Kisa na maana alizindua albamu ambayo ilikuwa tayari imevujishwa kwa umma kama ilivyokuwa na albamu ya Lil Wayne kwa jina ‘Tha Carter v mwaka 2016 na mwaka 2017.

Albamu ya Trippie Redd kwa jina ‘Pegasus’ ilizinduliwa rasmi tarehe 30 mwezi Oktoba mwaka huu wa 2020 lakini kazi yote ilikuwa tayari imevujishwa mwezi Agosti ambapo mashabiki wake walipata kusikiliza nyimbo zote 26.

Katika nyimbo hizo amehusidha wasanii wengine kama vile Wayne, Future, Young Thug, Quavo na wengine.

Albamu ya Wayne ‘Tha Carter V’ ilikwamishwa kwa muda mrefu kutokana na uhusiano uliozorota kati yake na Birdman na kampuni ya muziki kwa jina ‘cash money records’.

Mwaka 2017 Wayne, kampuni yamuziki ya Universal Records na ile ya Cash Money waliafikia makubaliano na wakampa uhuru wake kuondoka humo na akalipwa zaidi ya dola milioni kumi.

Lakini kabla azindue kazi hiyo yake rasmi, Martin Shkreli alikuwa tayari amejulikanisha baadhi ya vibao kwenye albamu hiyo.

Martin alitoa video iliyomwonyesha akiwa anaskiliza wimbo mmoja kwa hiyo albamu unaojulikana kama “Mona Lisa”.

Lil Wayne na mawakili wake walikuwa na nia ya kumshtaki Shkreli lakini wakamalizia kumpa maagizo makali ya kusita kujihusisha na kazi ya Wayne na kwamba asalimishe nakala aliyokuwa nayo ya albamu ya Wayne.

Hata hivyo Shkreli alijitetea akisema alinunua albamu hiyo na anaamini aliipata kwa njia halali kutoka kwa mtu anayedhaniwa kuwa mdukuzi wa mitandao.

Mwishowe albamu hiyo “Tha Carter v” ilizunduliwa mwezi Septemba mwaka 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *