Tobias Otieno ajiunga na Wanyama kupiga soka ya kulipwa Marekani

Kiungo wa timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka  23  Tobias  Otieno amekamilisha uhamisho hadi kilabu ya Union Omaha inayoshiriki  League One nchini Marekani.

Otieno  aliye na umri wa miaka 21 alikamilisha uhamisho wake hadi Marekani kutoka   Gor Mahia  mapema Januari mwaka huu ,lakini janga la  covid 19 likachelewesha mkataba huo.

Otieno akivalia jezi nambari tano katika timu ya Union Omaha Sc

Kiungo huyo  alijiunga na Kogalo mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2019/2020 baada ya kuwa na msimu wa kufana na Sony Sugar msimu wa mwaka 2018/2019 na kuisaidia Sony kutwaa nafasi ya tano ligini.

Tobias Otieno akiwa na kocha wake wa Union Omaha Sc Jay Mims

Union Omaha imezoa pointi  16 kutokana na mechi  10 walizosakata kushinda michuano minne kwenda sare minne na kupoteza mechi mbili  ,kufunga mabao 11 na kufungwa 11.

Otieno akiwa na wachezaji na maafisa wa kiufundi katika timu ya Union Omaha Sc

Otieno anajiunga na kapteni wa Harambee stars  Victor Wanyama  anayesakata soka ya kulipwa nchini Marekani  katika ligi kuu  League (MLS) akiwa na  Montreal Impact aliyojiunga nayo mwezi Machi mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *