Timu ya marathon ya olimpiki yapata ufadhili wa sh Milioni 1

Timu itakayowakilisha Kenya katika mbio za marathon kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo Japan baina ya julai na Agosti mwaka huu imepokea ufadhili wa shilingi milioni 1 kupiga kambi ya mazoezi kujiandaa kwa mashindano hayo

Timu ya marathon kwa michezo ya Olimpiki inawajumuisha bingwa mtetezi kwa wanaume Eliud Kipchoge, mshindi wa nishani ya shaba ya dunia mwaka 2019 Amos Kipruto, bingwa wa Boston na Chicago Marathon Lawrence Cherono, na bingwa wa Vienna City marathon Vincent Kipchumba .

Wanawake watakaolekea Tokyo Japan ni pamoja na bingwa wa dunia Ruth Chepngetich,bingwa mara mbili wa Londona marathonna mshikikizi wa rekodi dunia Brigid Kosgei, Ruth Chepngetich ,bingwa wa dunia na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya nusu marathon Peres Jepchirchir na bingwa wa Olimpiki katika mita 5000 mwaka 2016 Vivian Cheruiyot.

kutoka kushoto , naibu kiongozi wa timu ya Kenya SHoaib Vayani, koingozi wa timu ya kenya Waithaka Kioni, Rais wa NOCK Paul Tergat, Ruth Chepngetich, Meneja wa Kenya Barnaba Korir na meneja wa timu ya riadha ya kenya Ben Njoga

Rais wa kamati ya Olimpiki Kenya Paul Tergat ametoa hakikisho kuwa timu hiyo itapata usaidizi wote na maandalizi wanayohitaji kwa mashindano hayo.

“Kama NOCK tutahakikisha timu inapata mavazi ya kutosha na kwa wakati ufaao ,hatutaki kuwa na vijisababu Olimpiki ni mashidnnao muhimu hata mimi nimekuwa huko kwa wakati mmoja na nafahamu hisia ambazo mwanariadha huwa nazo” akasema Tergat

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *