Timu 8 kushiriki msururu wa kwanza wa Wadau Premier league

Timu 8 zimetoa ithibati kushiriki msururu wa kwanza wa mashindano ya Wadau Premie League Jumamosi Februari 27 katika uwanja wa michezo wa chuo cha Strathmore .

Akizungumza wakati wa uzinduliza ,mshirikishi wa mashindano hayo Bob Otieno amesema kuwa mashindano hayo yatawashirikisha wachezaji wanagenzi au wasio wa kulipwa na yatakuwa yakiandaliwa kila wakati wa likizo ambapo msururu wa pili unatarajiwa kuandaliwa wakati wa siku kuu ya pasaka mwezi April mwaka huu.

“Kile tunafanya tumeanza na timu 8 na zote ni za wachezaji wasio wa kulipwa ,baadae tutakuwa na msururu wa pili siku kuu ya pasaka” akasema Otieno
Mashindano hayo yanaandaliwa chini ya kauli mbiu ya ‘fans for fun’ ambapo zaidi ya mashabiki 500 wa timu hizo nane wanatarajiwa kuhudhuria mashindano hayo ya siku moja .

“tutaruhusu mashabiki wapatao 500 kuingia uwanjani Strathmore kwa kuzingatia masharti ya serikali kuhusu Covid 19 ” akaongeza Otieno

Kapteni wa zamani wa Harambee Stars Musa Otieno ambaye ni balozi wa mashindano hayo amesema dhamira yao ni kuonyesha mchango wa wachezaji wastaafu wa Kenya walio nchini na mataifa ya kigeni kukuza na kuinua vipaji.

“Haya ni mashandano mazuri ambayo yamedhaminiwa na wachezaji wastaafu wa Kenya waliokuja pamoja kuinua na kukuza vipaji “akasema Otieno

Wakati huo huo Otieno ambaye ni kapteni w amuda mrefu wa Harambee stars ametoa wito kwa FKF kuweka mikakati ya kukuza vipaji vya chipukizi kupitia mashindano ya shule ili kuinua viwango vya soka sawa na majirani Rwanda,Uganda na Tanzani ambao timu zao zilifuzu kwa mashindano ya CHAN na yale ya Afcon U 20 NA aFCON U 17.

“FKF inahitaji kuwekeza zaidi katika mashindano ya chipukizi na haswa ya shule ndio tuwe kiwango sawa na majirani zetu katika mashindano ya chipukizi Afrika”akaongeza Otieno

Mchezaji wa zamani wa Sofapaka Ronald Okoth ambaye ni mshirikishi wa shirika la Komborah ambalo linatoa mipira itakayotumiwa kwa mashindano hayo amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wachezaji walio nje ya nchi kukuza talanta na kuinua viwango vya mchezo.

Timu zitakazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Hippos,Tigers,Simba,Ndovu,Mafisi,Kulundeng Original ,Swara na Kulundeng.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *