Timu 60 kutoka Dagoretti Kusini kushiriki mashindano ya JamboBet
Jumla ya timu 60 kutoka eneo bunge la Dagoretti Kusini ,zimetoa ithibati kushiriki makala ya kwanza ya mashindano ya soka ya JamboBet yatakayoanza tarehe 15 mwezi huu huku fainali ikipigwa Desemba 13 mwaka huu.
Mashindano hayo yanaandaliwa na kampuni ya kamari ya JamboBet kwa ushirikiano na wasimamizi wa halmashauri ya uwanja wa Riruta .

Lengo la mashindano hayo ni kuziwezesha jamii za kutoka eneo bunge la Dagoretti South kupitia soka ,usafishaji mazingira , ushauri nasaha kwa vijana kuhusu jinsi ya kushiriki mchezo wa kamari kwa njia ya ustaarabupamoja na kutoa vyakula kwa jamii maskini kutoka eneo bunge hilo.

Kulingana na waandalizi wa mashindano hayo JamboBet ,wanalenga kueneza mashindano hayo katika kila eneo bunge kutoka kaunti 47 humu nchini.