Timu 40 zinashiriki mashindano ya Kabeabea Tigania East

Zaidi ta timu 40  za wanaume kutoka eneo bunge la Tigania mashariki zinashiriki makala ya kwanza ya mashindano ya Kabeabea  yaliyozinduliwa wikendi iliyopita katika uwanja wa Nguthiru .

Akizungumza wakati wa uzinduzi ,mbunge wa Tigania East Josphat Gichunge Kabeabea ambaye anafadhili mashindano hayo, aliwarai vijana kutumia fursa hiyo kuonyesha vipaji vyao vya soka huku maskauti kutoka FKF wakialikwa kutambua talanta .

Mbunge wa Tigania East  Josphat Kabeabea akizundua mashindano mwishoni mwa Juma

“Nimegundua kuwa tuna talanta nyingi za soka hapa Tigania East ambazo hazijatambuliwa ,na ndio maana nimeandaa mashindano haya ili kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuchukuliwa na maskauti ya Fkf na kwenda kuchezea timu kubwa”akasema Kabeabea

Sare za kuchezea na mipira iliyotolewa kwa timu washiriki

Mashindano hayo yatachezwa kwa njia ya mwondoano ,huku fainali ikipigwa Disemba 31 mwaka huu, kabla ya kutoa fursa kwa ligi ya fkf itakayoandaliwa kwa mara ya kwanza katika eneo bunge hilo baina ya Januari na Disemba mwaka ujao kama nji moja ya kukuza soka ,kutambua na kukuza talanta za mashinani.

“Baada ya mashindano haya tumeshirikiana na Fkf kuandaa ligi ya eneo bunge itakayoandaliwa kati ya Januari jna Disemba mwaka ujao ,ili tutambue na kukuza vipaji vya vijana wet una pia kuinua viwango vya soka huku mashinani”akaongeza Kabeabea

Mbunge huyo alitoa sare za kuchezea na mipira kwa kila timu inayoshiriki mashindano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *