Taswira ya vifo vya wanaspoti mwaka 2020

Mwaka 2020 umeshuhudia magwiji wengi wa michezo wakiaga dunia kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa nyota wa michezo waliofariki ni mchezaji  wa zamani wa Senegal  Pope Diouf  ambaye alihudumu kama Rais wa klabu ya  Olympiaue Marseille aliaga dunia mwezi April akiwa na umri wa miaka 68 kutokana na ugonjwa wa Covid 19 .

Akiwa Rais wa Marseille kati ya mwaka 2005 na 2009  timu hiyo ilimaliza ya pili, mara mbili katika ligi kuu Ufaransa  na kucheza fainali mbili za kombe la Ufaransa .

Pope Diouf

Paolo Rossi, mchezaji aliyekuwa katika kikosi cha Italia kilichotwaa kombe la dunia mwaka 1982 pia alifariki mapema Disemba mwaka huu akiwa na umri  wa  miaka 64.

Paolo Rosi

Gerard Houllier wa Ufaransa ambaye pia alikuwa meneja wa zamani wa Liverpool aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 73 ,na kiwa meneja wa Liverpool kati ya mwaka 1998 na 2004 alitwaa mataji matatu.

Gerrard Houlier

Nahodha wa Cameroon miaka ya 90 Stephen Tataw pia alifariki ,na atakumbukwa  wakiwa pamoja na  Roger Milla na Francois Omam-Biyik,kwenye fainali za kombela dunia Indomitable Lions ikicheza hadi robo fainali .

Stephen Tataw

Mchezaji wa zamani wa  timu Afrika Kusini  Anele Ngongca pia alifariki kupitia ajali ya barabarani.

Ulimwengu pia uliomboleza kifo cha  nyota wa mpira wa kikapu  Kobe Bryant  aliyekuwa na umri wa miaka 41 ,aliyeangamia kwenye ajali ya ndege akiwa na binti yake .

Kobe Bryant

Mwezi Novemba pia kiungo mkabaji  wa Senegal kwenye kombe la dunia mwaka 2002 Papa Bouba Dioup alifariki akiwa na umri wa miaka 42.

Pia Disemba beki wa kati wa klabu ya Mamelodi Sundowns Motjeka Madisha alifariki kupitia ajali ya barabarani akiwa na umri wa miaka 25.

Diop baada ya kufunga bao mwaka 2002  dhidi ya Ufaransa

Nyota wa Argentina  Diego Maradona  alifariki   Novemba 25 akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kuugua kwa muda kutokana na sababu kadhaa.

Maradona anakumbukwa kwa bao alilofunga kwa mkono katika robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Uingereza mwaka 1986 akiwa nahodha na pia kusaidia kuishinda Ujerumani Magharibi kwenye fainli.

Diego Maradona

Nchini Kenya nyota wa michezo walioangamia ni kama:-

Beki  Tonny Onyango mchezaji raga wa kilabu cha KCB  alifariki akiwa na umri wa miaka 28 baada ya kuanguka na kufariki akiwa nyumbani kwake Ngong mapema mwezi Machi mwaka huu .

Hadi kifo chake Onyango alichezea timu za taifa kwa chipukizi kabla ya kuteuliwa kuichezea timu ya taifa kwa wachezaji 15 kila upande Simbas mwaka 2012.

Tonny Onyango

Charles Oguk mchezaji hoki wa timu ya taifa  aliyeshiriki Olimpiki mwaka 1988 alifariki akiwa na umri wa miaka 56 .

Uguk pia alishiriki michezo ya bara Afrika mwaka 1987 jijini Naiorobi na kuisaidia timu hiyo kutwaa medali ya fedha.

Taifa pia lilimpoteza kocha wa soka  Henry Omino mara ya mwisho akiifunza Western Stima , aliyefarifiki mwezi Machi akiwa na umri wa miaka  71 kutokana na saratani na alikuwa amefanya ukufunzi tangu mwaka  1975.

Henry Omino

Mshambulizi wa zamani wa Harambee Stars  na Gor Mahia ,Martin Ouma maarufu kama Ogwanjo alifariki mwezi Mei akiwa na umri wa miaka  71 kutoka na kiharusi,akiwa kwenye timu iliyoshiriki fainali za Afcon mwaka 1972 nchini Cameroon.

Pia sekta ya Soka ilimpoteza Suleiman Khamisi Shamba, beki wa zamani wa Harambee Stars akiwa na umri wa miaka 62 kutokana na matatizo ya figo .

Alikuwa kwenye kikosi cha Kenya kilichonyakua kombe la Cecafa miaka 1981,83 na 85.

Katika Mwezi Agosti pia Kevin Oliech kakake mdogo Dennis Oliech alifariki nchini Ujerumani kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 31.

Katika enzi zake alichezea timu za Mathare United,Tusker Fc,Nairobi City Stars,Thika United,Ushuru Fc,Nakumatta Fc  na Gor Mahia huku akichukua ubingwa wa ligi na mathare mwaka 2008.

Kevin Oliech

Raga pia ilimpoteza Allan Makaka, akiwa na umri wa miaka 38 baada ya wing’a huyo kuhusika katika ajali barabarani .

Hadi kifo chake alikuwa amechezea timu za Ulinzi na Herlequins na pia timu ya wachezaji iliyoshiriki kombe la dunia mwaka 2005 na michezo ya jumuiya ya madola ,mwaka 2006.

Allan Makaka

Dickson Wamwiri, mchezaji Taekwondo aliyeshiriki michezo ya Olimpiki mwaka 2008  na kunyakua dhahabu katika michezo ya Afrika mwaka 2007 aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 35

Ben Jipcho gwiji wa riadha alifariki Julai 24 katika Hospitali ya Fountain mjini Eldoret kutoka na viungo vyake vingi mwilini kudinda kufanya kazi.

Ben Jipcho

Jipcho alianza riadha mapema miaka ya 60 na aliishindia Kenya dhahabu katika mita  5000 michezo ya Afrika mwaka 1973  na dhahabu katika michezo ya jumuiya ya madola mwa 74 mbio za mita 5000 na mita 3000 kuruka viunzi na maji na shaba ya mita 1500.

Rosemary “Mara” Aluoch, kipa wa zamani wa timu ya soka ya wanawake ya Kenya aliaga akiwa na umri wa miaka  44 na anakumbukwa kuichezea Harambee starlets baina ya mwaka 1995 na 2012.

Rosemary Aluoch Mara

Mshindi mara 4 wa mashindano ya gofu ya Kenya Open Edward Legei, alifariki Novemba akiwa na umri wa miaka  56.

Mohammed  Hatimy aliyekuwa Rais wa shirikisho la soka nchini baina ya mwaka 2005 na 2011 alifariki Novemba 14 kutokana na ugonjwa wa Covid 19 .

Mohammed Hatimy

Meneja wa muda mrefu wa klabu ya Nairobi City Stars Neville Pudo,alifariki akiwa na umri wa miaka  63 akiwa nyumbani kwake .

Nevile Pudo

Kwa jumla mwaka 2020 tumewapoteza wanamichezo wengi kwa sababu mbalimbali lakini pia gonjwa la Covid 19 limechangia kwa idadi ya vifo hivyo.

Kunao nyota wengine wa michezo ambao sijawataja lakini kwa familia za wanamichezo wa Kenya waliotuacha mwaka 2020 ,,,,,,,Makiwa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *