Taswira ya matukio makuu ya soka 2020

Mwaka 2020 umekuwa na matukio machache ya soka kuliko ilivyotarajiwa kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Covid 19 .

Barani Afrika  mashindano ya kombe la CHAN yalipaswa kuandaliwa mwezi April nchini Cameroon,pia fainali za kombe la Euro barani Ulaya  na mashindano mengine makuu yakiahirishwa hadi mwaka ujao.

Sadio Mane wa Senegal na Liverpool ,alitawazwa mwanasoka bora Afrika kwa mara ya kwanza mapema Januari.

Hata hivyo Ligi nyingi za bara Afrika na mabara mengine zilifutiliwa mbali huku chache zikiahirishwa .

Nchini Kenya msimu wa ligi kuu ulifutiliwa mbali huku Gor Mahia wakitawazwa mabingwa baada ya mechi 23 pekee  wakiwa na  alama 54.

Pia mechi za Harambee Stars za Kundi  G kufuzu kombe la AFCON zilizokuwa zichezwe mwezi Machi dhidi ya Comoros nyumbani na ugenini zilisongezwa mbele hadi Novemba mwaka huu  Kenya wakipoteza nafasi ya kufuzu baada ya kutoka sare  ya 1-1 nyumbani kabla ya kushindwa 1-2 ugenini .

Mechi mbili za mwisho kuchezwa Machi mwaka ujao Kenya ikihitaji kushinda mechi zote na kutarajia kuwa Misri na Comoros wanaongoza kundi hilo  watakosa kuzoa pointi.

Kenya inasalia kuanza kujipanga kwa mechi za kufuzu kwenda Afcon ,mwaka 2023 kwani hawana fursa ya kufuzu kwenda Cameroon mwaka 2022.

Ligi kuu ya Soka  msimu wa mwaka 2020/2021 hatimaye  ilianza Novemba 28 ikifuatwa na ligi ya Nsl wiki moja baadae na ligi kuu ya Wanawake.

Soka ya bara Afrika ilishuhudia klabu ya RS Berkane ya Moroko ikitawazwa mabingwa wa kombe la shirikisho kwa mara ya kwanza kwa kuwashinda Pyramids kutoka Misri  bao 1-0  mwezi Oktoba wakati Al Ahly  ya Misri ikiwazidia maarifa Zamalek  2-1 na kunyakua kombe la ligi ya mbingwa Afrika  kwa mara ya 9 .

Barani Ulaya Bayern Munich walishinda kombe la ligi ya mabingwa kwa mara ya 6 ,baada ya kuwaangusha PSG bao  1-0 wakati Seville wakishinda Europa League kwa kuinyuka Intermilan  3-2 na kushinda kombe hilo kwa mara ya 6.

Rais wa CAF Ahmad Ahmad alipigwa marufuku ya miaka mitano  na kitengo cha maadili cha FIFA  mwezi Novemba kwa makosa kadhaa ya ufisadi na matumizi mabaya ya Afisi.

Ligi mbalimbali za mabara yote hatimaye zilirejelewa au kuanza upya huku  pia bara Amerika kusini likicheza mechi nne za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2022 baina ya Oktoba na Novemba.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *