Categories
Michezo

Tanzania yapigwa kumbo huku Moroko walilazimisha ushindi AFCON U 20

Timu ya Ghana kwa wanaume wasiozidi umri wa miaka 20 illinyuka Tanzania maarufu kama ngorongoro Heroes  mabao 4-0 katika mkwangurano wa kundi C kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mjini Noukchot nchini Mauritania Jumanne usiku.

Precious Boah alipachika mabao mawili kwa Ghana maarufu kama  Black Satellites  ,kabla ya Abdul Fatawu na Joselpho Barnes  kuongeza mengine mawili.

Katika pambano jingine  Moroko walihitaji penati tatanishi kunako kipindi cha kwanza ili kuwashinda Gambia bao 1-0 .

Mashindano hayo kuendelea Jumatano kwa mechi mbili za kundi A  Cameroon na Uganda wakimenyana katika mechi ya kwanza saa moja usiku huku atakayeshinda akifuzu kwa kwota fainali na pia sare itatosha kuvusha timu zote mbili kwa robo fainali baada ya kushinda mechi zao za ufunguzi.

Katika mechi ya pili kundini humo Msumbiji watachuana na wenyeji Mauritania saa nne usiku huku atakayeshindwa akiyaaga mashindano ,hususan baada ya wote wawili kupoteza mechi za ufunguzi.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *