Tanzania yapendelea madawa ya kienyeji kuliko chanjo za kigeni kukabiliana na korona

Waziri wa Afya nchini Tanzania Dorothy Gwajima amesema taifa hilo halina mipango ya kuagiza chanjo za kigeni za ugonjwa wa COVID-19.

Waziri huyo badala yake amewahimiza raia wa nchi hiyo kutumia madawa ya kienyeji kama njia moja ya kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limechukua msimamo huo wakati huu ambapo kuna hofu kuwa maambukizi ya virusi vya korona yanaongezeka.

Aidha, Gwajima ameonya mashirika ya habari dhidi ya kuchapisha habari zisizo rasmi kuhusiana na maambukizi ya virusi hivyo.

Tanzania ni moja wapo wa mataifa machache duniani ambayo hayachapishi takwimu kuhusu maambukizi ya virusi hivyo.

Mwezi uliopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilihimiza Tanzani kufikiria kuwachanja raia wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *