Tanasha Donna aomba usaidizi kwa niaba ya meneja wake

Mwanamuziki, mtangazaji na mwanamitindo wa nchi ya Kenya Tanasha Donna kupitia akaunti yake ya Instagram, aliomba usaidizi kwa niaba ya African Castro ambaye ni meneja wake.

Donna aliomba mashabiki wake mchango ili kusaidia kulipa ada ya hospitali ya babake African Castro ambaye aliugua na kulazwa na baadaye kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Castro kupitia akaunti yake ya instagram alielezea kwamba, babake anaugua kisukari ugonjwa ambao ulisababishwa akatwe sehemu ya mguu wake na alipolazwa pia akachukuliwa kama mgonjwa wa Covid !9 kulingana na dalili alizokuwa nazo.

Meneja huyo wa Tanasha anaendelea kuelezea kwamba mzazi huyo alipata nafuu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini ila bili bado haijalipwa kwa kikamilifu.

Tanasha alielezea kwamba yeye, watu wake wa karibu na hata African Castro wanafanya kila wawezalo kumaliza deni hilo lakini ni kubwa mno na wanahitaji kusaidiwa.

Anaelezea kwamba kwa sasa bili hiyo ni milioni saba na kwa wale ambao wangetanga kusaidia, alitoa maelezo ya kufanya vile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *